Nyumbani

RAIS WA VYUO VYA BAHARI DUNIANI AIPONGEZA NEMC KWA USIMAMIZI ENDELEVU WA MAZINGIRA

Rais wa Vyuo vya Masuala ya Bahari (Word Maritime University) Duniani, Profesa Maximo Q. Mejia, Jr amelipongeza Baraza la Taifa la Hifadhi na Usimamizi wa Mazingira (NEMC) kwa usimamizi wa Mazingira nchini yenye kuleta Mazingira wezeshi katika sekta ya uchumi wa buluu

Profesa Maximo ametoa pongezi hizo Septemba 8, 2026 alipotembelea Banda la NEMC kwenye Kongamano la 5 la Kimataifa la Uchumi wa Buluu linalofanyika katika Ukumbi wa Mikutano wa Kimataifa wa Julius Nyerere (JNICC) kuanzia Septemba 7 hadi 9, 2026.

Kongamano hilo lililofunguliwa rasmi na Waziri wa Nchi, Ofisi ya Makamu wa Rais (Muungano na Mazingira), Mhe. Mhandisi Hamad Yusuf Masauni akimwakilisha Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Deogratius Ndejembi, linakwenda sambamba na kaulimbiu isemeyo “Powering Blue Initiatives for Sustainable Economic Growth in Africa”.

NEMC katika Kongamano hilo imejipambanua katika sekta ya mazingira kwa kusisitiza umuhimu wa matumizi endelevu ya rasilimali za bahari, mito, maziwa na maeneo ya Pwani, sambamba na uhifadhi na usimamizi endelevu wa mazingira.

Baraza la Taifa la Hifadhi na Usimamizi wa Mazingira (NEMC) Kanda ya Mashariki Kusini limeshiriki kikao kazi kuhusu tahadhari za Mvua za El ñino katika wilaya ya Mafia kilichofanyika tarehe 8 Septemba 2026 katika ukumbi wa Hamshauri  ya Wilaya ya Mafia.

Kikao kilihusisha wataalamu kutoka NEMC, Halmashauri ya Wilaya ya Mafia pamoja na Maafisa Tarafa ambapo kilijadili hatua mbalimbali zinazopaswa kuchukuliwa katika kujiandaa na kukabiliana na athari zinazoweza kujitokeza kutokana na mvua hizo.

Hatua hizo ni pamoja na kuimarisha kamati ya Maafa ya Wilaya pamoja na kamati za maafa ngazi za kata na vijiji, utoaji wa elimu kwa wananchi juu ya tahadhari za kuchukua, kuimarisha udhibiti wa taka ngumu na usafi wa mazingira, usafishaji wa mitaro, kuhamasisha wananchi kuweka akiba ya chakula na nishati (mkaa au gesi) majumbani, kuimarisha timu za uokozi, kuhamasisha wananchi kuondoka maeneo hatarishi kama vile mabondeni na kuzingatia taarifa za tahadhari zinazotolewa na Mamlaka ya Hali ya Hewa Tanzania.

#nemc

#ofisiyamakamuwarais

#tma

#elniño

#mazingirayetuuhaiwetu

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni

NEMC YAKUTANA NA KAMATI YA KUDUMU YA BUNGE YA BAJETI

Baraza la Taifa la Hifadhi na Usimamizi wa Mazingira (NEMC) limekutana na Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Bajeti na kujadili utekelezaji wa baj...