Nyumbani

NEMC YASHIRIKI KONGAMANO LA 11 LA BELT AND ROAD SUMMIT JIJINI HONG KONG-CHINA

Baraza la Taifa la Hifadhi na Usimamizi wa Mazingira NEMC limeshiriki Kongamano la kumi na moja (11) la kuhamasisha uwekezaji la "𝑩𝒆𝒍𝒕 𝒂𝒏𝒅 𝑹𝒐𝒂𝒅 𝑺𝒖𝒎𝒎𝒊𝒕" lililofanyika kuanzia tarehe 9 hadi 11 Septemba 2026 katika kituo cha Mikutano cha Hong Kong convention Center Jijini Hong Kong nchini China.

Kongamano hilo limewakutanisha zaidi ya wadau 6,000 wakiwemo viongozi wa serikali na wafanyabiashara wakubwa kwa lengo la kukuza na kuimarisha ushirikiano wa kibiashara, kiuchumi, na uwekezaji wa kimataifa.

NEMC kama Taasisi inayosimamia Mazingira nchini imeishiriki Kongamano hilo ili kukutana na kujifunza fursa za uwekezaji na uendeshaji wa miradi ya kimkakati inayozingatia Sheria na Kanuni za Uhifadhi na Usimamizi wa Mazingira kwa maendeleo endelevu. Aidha wajumbe wengine kutoka Tanzania walioshiriki Kongamano hilo ni TISEZA, TANESCO, TBA na TEMESA

Aidha wajumbe kutoka NEMC walipata fursa ya kutembelea wadau na wafanyabiashara wakubwa waliojumuika katika maonesho ya Kongamano hilo ili kujifunza na kujionea Teknolojia na uwekezaji unaozingatia Uhifadhi na Usimamizi wa Mazingira wakiwemo BEAM Society LTD, Sanfeng Environment "For a Cleaner World" na Allied Environmental Consultants

Kongamano la 11 la Belt and Road Summit kwa mwaka 2026  lilibeba kaulimbiu isemayo "𝐀𝐝𝐯𝐚𝐧𝐜𝐢𝐧𝐠 𝐇𝐢𝐠𝐡-𝐐𝐮𝐚𝐥𝐢𝐭𝐲 𝐃𝐞𝐯𝐞𝐥𝐨𝐩𝐦𝐞𝐧𝐭 · 𝐄𝐦𝐛𝐚𝐫𝐤𝐢𝐧𝐠 𝐨𝐧 𝐚 𝐍𝐞𝐰 𝐉𝐨𝐮𝐫𝐧𝐞𝐲" likiangazia zaidi ushirikiano wa kibiashara, uwekezaji, na maendeleo mapya.

Mwakilishi wa heshima (Tanzania) wa eneo Maalum la Kiutawala la Jamhuri ya watu wa China la Hong Kong (Special Administrative Region (SAR) Mhe. Leung Tin Fu wa tatu kutoka kulia akiwa katika picha ya pamoja na wajumbe kutoka Tanzania walioshiriki Kongamano la kumi na Moja (11) la kuhamasisha uwekezaji la 𝑩𝒆𝒍𝒕 𝒂𝒏𝒅 𝒓𝒐𝒂𝒅 𝒔𝒖𝒎𝒎𝒊𝒕 lililofanyika katikati Kituo cha Mikutano cha Hong Kong Conference Convention center kuanzia tarehe 9 hadi 11 Septemba 2026 Jijini Hong Kong nchini China.










 

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni

NEMC YAKUTANA NA KAMATI YA KUDUMU YA BUNGE YA BAJETI

Baraza la Taifa la Hifadhi na Usimamizi wa Mazingira (NEMC) limekutana na Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Bajeti na kujadili utekelezaji wa baj...