Nyumbani

WAZIRI MKUU ATOA TUZO KWA VIONGOZI NA WADAU WA MAZINGIRA KATIKA MAADHIMISHO YA MIAKA 40 YA NEMC

 Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Mwigulu Lameck Nchemba akikabidhi Tuzo kwa Viongozi, Wadau wa mazingira na Washindi wa mazingira challenge katika Kongamano la Kisayansi lililoandaliwa na Baraza la Taifa la Hifadhi na Usimamizi wa Mazingira (NEMC) ikiwa ni sehemu ya Maadhimisho ya Miaka 40 ya NEMC lililofanyika katika Ukumbi wa Mikutano wa Julius Nyerere (JNICC), Jijini Dar es Salaam.









WAZIRI MKUU DKT. MWIGULU NCHEMBA AKABIDHIWA TUZO YA HESHIMA NEMC@40

 Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Mwigulu Nchemba akikabidhiwa Tuzo mnaalum na Waziri wa Nchi, Ofisi ya Makamu wa Rais (Muungano na Mazingira) Mhe. Mhandisi Hamad Yusuf Masauni ikiwa ni ishara ya kutambua mchango wake katika Uhifadhi na Usimamizi wa Mazingira nchini.

 


Tuzo hiyo ilikabidhiwa wakati wa Kongamano la Kisayansi lililoandaliwa na Baraza la Taifa la Hifadhi na Usimamizi wa Mazingira (NEMC) ikiwa ni sehemu ya Maadhimisho ya Miaka 40 ya NEMC lililofanyika katika Ukumbi wa Mikutano wa Julius Nyerere (JNICC), Jijini Dar es Salaam.

 

WAZIRI MKUU DKT. MWIGULU NCHEMBA AHUTUBIA KONGAMANO LA KISAYANSI NEMC@40

 



Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Mwigulu Lameck Nchemba (Mb) akihutubia wakati wa Kongamano la Kisayansi lililoandaliwa na Baraza la Taifa la Hifadhi na Usimamizi wa mazingira (NEMC) ikiwa ni sehemu ya Maadhimisho ya Miaka 40 ya NEMC.
























WAZIRI MKUU AZINDUA MFUMO WA TOCEMS KATIKA KONGAMANO LA MAZINGIRA NEMC@40

Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mwigulu Nchemba, amezindua Mfumo wa Kidigitali wa Kufuatilia Uchafuzi wa Mazingira (TOCEMS) wakati wa Kongamano la Kisayansi la Maadhimisho ya Miaka 40 ya Baraza la Taifa la Hifadhi na Usimamizi wa Mazingira (NEMC). Katika hafla hiyo, Dkt. Nchemba alimpongeza NEMC kwa juhudi kubwa na mafanikio ya miongo minne katika Uhifadhi na Usimamizi wa Mazingira nchini.

Kongamano hilo lilifanyika Mei 28, 2026, katika Ukumbi wa Kimataifa wa Mikutano wa Julius Nyerere (JNICC) jijini Dar es Salaam, likiwa na kaulimbiu “NEMC@40: Tunza Mazingira, Linda Taifa.” Lengo kuu lilikuwa kujadili mchango wa usimamizi wa mazingira katika maendeleo endelevu ya Taifa pamoja na kutafuta suluhisho la changamoto mbalimbali za kimazingira zinazoikabili nchi.

Akizungumza na wajumbe, Dkt. Nchemba alisisitiza kuwa Serikali itaendelea kuimarisha ushirikiano na NEMC ili kuhakikisha sheria, kanuni na miongozo ya mazingira inatekelezwa ipasavyo katika sekta zote za maendeleo. Alibainisha kuwa uhifadhi wa mazingira si jukumu la taasisi moja pekee, bali ni wajibu wa kila mwananchi na kila sekta kwa mustakabali wa Taifa na vizazi vijavyo. Aidha, Serikali inaendelea kuchukua hatua za kukabiliana na mabadiliko ya tabianchi na kudhibiti shughuli zinazosababisha uharibifu wa mazingira

Mfumo wa TOSEMS uliozinduliwa unalenga kuimarisha usimamizi na ufuatiliaji wa shughuli zinazoweza kusababisha uchafuzi wa mazingira nchini. Dkt. Nchemba alieleza kuwa mfumo huo utaongeza ufanisi katika ukusanyaji wa taarifa, ufuatiliaji wa viashiria vya uchafuzi na kurahisisha utoaji wa taarifa kwa mamlaka husika ili kuchukua hatua za haraka. Hatua hiyo inatarajiwa kuboresha uwazi na uwajibikaji katika usimamizi wa mazingira.

Waziri wa Nchi, Ofisi ya Makamu wa Rais (Muungano na Mazingira), Mhe. Mhandisi Hamad Yusuf Masauni, aliahidi kuwa Serikali itaendelea kushirikiana na wadau mbalimbali kuhakikisha rasilimali za Taifa zinalindwa kwa manufaa ya kizazi cha sasa na kijacho. Kwa upande wake, Mkurugenzi Mkuu wa NEMC, Dkt. Immaculate Sware Semesi, alisema katika miaka 40 Baraza limefanikiwa kuimarisha usimamizi kupitia tafiti, elimu kwa umma, tathmini za athari za mazingira na ukaguzi wa miradi. Mafanikio hayo, alisema, yametokana na ushirikiano kati ya Serikali, sekta binafsi, wadau wa maendeleo na wananchi.

Kongamano hilo limehudhuriwa na wadau mbalimbali kutoka Serikalini, sekta binafsi, mashirika yasiyo ya kiserikali, taasisi za elimu na wananchi, wote wakijadili matumizi ya teknolojia na mikakati ya kuimarisha usimamizi wa mazingira. Ni sehemu ya maandalizi ya kilele cha maadhimisho ya miaka 40 ya NEMC yanayotarajiwa kufanyika Mei 29, 2026. NEMC imeahidi kuendelea kuimarisha matumizi ya teknolojia, tafiti na kampeni za elimu ili kuhakikisha Tanzania inabaki na mazingira salama na endelevu kwa vizazi vijavyo.









SERIKALI YASISITIZA UWAJIBIKAJI WA MAZINGIRA KWA VIWANDA NA WADAU WA TAKA HATARISHI

Serikali imeendelea kusisitiza umuhimu wa kuzingatia sheria za mazingira kwa sekta ya viwanda, kampuni za uteketezaji taka pamoja na wadau wanaohusika na uhifadhi wa bidhaa hatarishi, ikiwa ni sehemu ya juhudi za kulinda afya za wananchi na kuhakikisha maendeleo endelevu ya taifa.


Hayo yamejadiliwa katika mkutano wa wadau wa mazingira ulioandaliwa na Baraza la Taifa la Hifadhi na Usimamizi wa Mazingira (NEMC), uliowakutanisha wamiliki wa viwanda, wateketezaji wa taka na wenye maghala ya bidhaa hatarishi kwa lengo la kujadili namna bora ya kuimarisha usimamizi wa mazingira nchini.


Akizungumza katika kikao hicho, Naibu Waziri wa Ofisi ya Makamu wa Rais (Muungano na Mazingira), Mheshimiwa Reuben Nhamanilo Kwagilya, amesema ukuaji wa sekta ya viwanda unapaswa kwenda sambamba na utekelezaji wa sheria za mazingira ili kupunguza athari zinazoweza kuhatarisha afya za wananchi na mazingira.


Alieleza kuwa mazingira ni msingi muhimu wa maendeleo ya kiuchumi na kijamii, hivyo kila mdau wa uzalishaji na usimamizi wa taka ana wajibu wa kuhakikisha shughuli zake zinafanyika kwa kuzingatia viwango vya usalama wa mazingira na afya.


Katika kikao hicho, Serikali ilisisitiza umuhimu wa utekelezaji wa Sheria ya Usimamizi wa Mazingira, ikiwemo udhibiti wa uchafuzi wa hewa, maji na ardhi unaotokana na shughuli za viwanda pamoja na usimamizi sahihi wa taka ngumu na taka hatarishi.


Aidha, wadau walikumbushwa umuhimu wa kufanya Tathmini ya Athari kwa Mazingira (EIA) kabla ya kuanza miradi ya maendeleo pamoja na kufanya ukaguzi wa mazingira mara kwa mara ili kuhakikisha shughuli za uzalishaji zinaendana na matakwa ya sheria.


Mkutano huo pia uliangazia changamoto zinazotokana na ongezeko la taka za viwandani na matumizi ya kemikali hatarishi, ambapo NEMC ilihimiza matumizi ya teknolojia safi na mifumo bora ya uteketezaji na urejelezaji taka ili kupunguza uchafuzi wa mazingira.


Katika kuimarisha usimamizi endelevu wa rasilimali, Serikali imeendelea kuhamasisha utekelezaji wa dhana ya Uchumi Mzunguko (Circular Economy) inayolenga kupunguza uzalishaji wa taka, kutumia tena bidhaa na kurejeleza malighafi kwa matumizi mengine ya kiuchumi.


Wadau wa mazingira walielezwa kuwa utekelezaji wa mfumo huo unaweza kusaidia viwanda kupunguza gharama za uzalishaji, kuongeza ufanisi wa matumizi ya rasilimali pamoja na kuongeza ushindani wa bidhaa katika soko la ndani na kimataifa.


Kwa upande wake, NEMC ilisisitiza kuwa ushirikiano kati ya Serikali, sekta binafsi na wataalam wa mazingira ni muhimu katika kuhakikisha Tanzania inakuwa na sekta ya viwanda inayozingatia sheria, inalinda mazingira na kuchochea ukuaji wa uchumi wa taifa.


Mkutano huo umetajwa kuwa jukwaa muhimu la kubadilishana uzoefu, kujadili changamoto zinazokabili wadau wa mazingira pamoja na kuibua mapendekezo yatakayosaidia kuboresha utekelezaji wa sheria za mazingira nchini.


Kupitia mikutano kama hiyo, Serikali inalenga kujenga uelewa mkubwa kwa wadau kuhusu umuhimu wa matumizi salama ya kemikali, uhifadhi sahihi wa bidhaa hatarishi, usimamizi wa taka na uwekezaji katika teknolojia rafiki kwa mazingira kwa ajili ya ustawi wa kizazi cha sasa na kijacho.



TAKA SI UCHAFU TENA: TANZANIA YAELEKEA UCHUMI WA KIJANI KUPITIA UREJELESHAJI

Katika hatua muhimu ya kuimarisha usimamizi wa mazingira na kukuza uchumi wa kijani nchini, Serikali kupitia Baraza la Taifa la Hifadhi na Usimamizi wa Mazingira (NEMC), imekutana na wadau wa usimamizi wa taka na urejelezaji jijini Dar es Salaam kujadili mustakabali wa sekta hiyo na nafasi yake katika maendeleo endelevu ya Taifa.

Kikao hicho kilichofanyika tarehe 13 Mei 2026 katika ukumbi wa NEMC – Mikocheni, kiliwakutanisha viongozi wa Serikali, wadau wa mazingira, waokota taka rejeshi, waokota chuma chakavu, sekta binafsi pamoja na wadau wa maendeleo kwa lengo la kujenga mfumo jumuishi wa usimamizi wa taka unaolinda mazingira na kuongeza thamani ya kiuchumi kupitia urejelezaji.

Akifungua kikao hicho, Naibu Katibu Mkuu (Mazingira), Ofisi ya Makamu wa Rais, Balozi Baraka Haran Luvanda alisema kuwa Tanzania kwa sasa huzalisha zaidi ya tani milioni 14.4 za taka ngumu kila mwaka, huku karibu nusu ya taka hizo zikizalishwa katika miji mikubwa kama Dar es Salaam, Mwanza, Arusha, Dodoma, Mbeya na Tanga. Alieleza kuwa iwapo taka hizo hazitasimamiwa vizuri zinaweza kusababisha madhara makubwa ikiwemo uchafuzi wa mazingira, magonjwa ya mlipuko, kuziba mifereji na mafuriko.

Hata hivyo, Serikali imebainisha kuwa taka si tatizo pekee bali pia ni rasilimali yenye uwezo mkubwa wa kuchangia uchumi wa Taifa kupitia dhana ya uchumi mzunguko (Circular Economy). Kupitia mfumo wa “Punguza, Tumia Tena na Rejeleza” maarufu kama 3Rs, Serikali inalenga kubadili mtazamo wa jamii ili kuona taka kama chanzo cha ajira, malighafi na maendeleo.

Katika hotuba yake, Balozi Luvanda aliwatambua waokota taka rejeshi na waokota chuma chakavu kama mashujaa wa kimya wanaochangia kwa kiwango kikubwa kupunguza taka zinazopelekwa dampo, kuongeza viwango vya urejelezaji na kusaidia kupunguza uzalishaji wa gesijoto. Alisisitiza kuwa kazi yao imekuwa nguzo muhimu katika kuimarisha uchumi wa kijani nchini.

“Waokota taka na waokota chuma chakavu ni sehemu muhimu ya mfumo wa usimamizi wa taka nchini. Kupitia kazi yao, maelfu ya vijana na wanawake wamepata ajira na kipato huku mazingira yakihifadhiwa,” alisema.

Kwa upande wake, Mkurugenzi Mkuu wa Baraza la Taifa la Hifadhi na Usimamizi wa Mazingira, Dkt. Immaculate Sware Semesi, alisema kuwa maadhimisho ya miaka 40 ya NEMC yenye kauli mbiu “NEMC@40: Tunza Mazingira, Linda Taifa” yanapaswa kuwa chachu ya kuongeza uwekezaji na ubunifu katika sekta ya usimamizi wa taka.

Aliyataja makundi mbalimbali kama Tanzania Waste Pickers Association (TAWAPA), Tanzania Recyclers Association(TARA) pamoja na Mtandao wa Waokota Taka Rejeshi Dar es Salaam (MTAWADA) kuwa miongoni mwa wadau muhimu wanaosaidia kusukuma mbele agenda ya uchumi mzunguko nchini.


Dkt. Semesi alibainisha kuwa NEMC imeendelea kushuhudia ongezeko la wawekezaji na taasisi zinazojihusisha na shughuli za ukusanyaji, usafirishaji, uchakataji na urejelezaji wa taka, hali inayodhihirisha kuongezeka kwa mwamko wa uzingatiaji wa sheria za mazingira pamoja na kukua kwa sekta ya uchumi mzunguko nchini.

Aidha, alieleza kuwa matumizi ya teknolojia za kisasa katika usimamizi wa taka, ikiwemo mifumo ya kidijitali ya ufuatiliaji wa taka, mashine za uchakataji pamoja na teknolojia za kuzalisha nishati kutokana na taka, yanafungua ukurasa mpya wa uwekezaji na ubunifu nchini Tanzania.


#NEMC40 #Miaka40YaNEMC #NEMCat40 #SustainableTanzania #MazingiraYetuUhaiWetu #MsemajiMkuuWaSerikali #2026Trends #SamiaSuluhuHassan#π‘΄π’‚π’›π’Šπ’π’ˆπ’Šπ’“π’‚π’€π’†π’•π’–π‘Όπ’‰π’‚π’Šπ‘Ύπ’†π’•π’– 

#TUNZAMAZINGIRALINDATAIFA

MWENYEKITI WA BODI YA NEMC AZUNGUMZA NA WADAU WA MAZINGIRA, NEMC@40

Mwenyekiti wa Bodi ya NEMC, Mhandisi Mwanasha Tumbo akizungumza wakati wa Maadhimisho ya Miaka Arobaini (40) ya Baraza la Taifa la Hifadhi n...