Nyumbani

MWENYEKITI WA BODI YA NEMC AZUNGUMZA NA WADAU WA MAZINGIRA, NEMC@40

Mwenyekiti wa Bodi ya NEMC, Mhandisi Mwanasha Tumbo akizungumza wakati wa Maadhimisho ya Miaka Arobaini (40) ya Baraza la Taifa la Hifadhi na Usimamizi wa Mazingira (NEMC) yaliyofanyika tarehe 29 Mei 2026 katika Ukumbi wa Mikutano wa Julius Nyerere (JNICC), Jijini Dar es Salaam.

Katika mazungumzo hayo, amesisitiza umuhimu wa ushirikiano wa wadau mbalimbali katika kulinda na kuhifadhi mazingira, akieleza kuwa mafanikio ya NEMC katika kipindi cha miaka 40 yamechangiwa kwa kiasi kikubwa na ushiriki wa serikali, sekta binafsi, taasisi na wananchi.

Aidha, ametoa wito wa kuendelea kuwekeza katika elimu ya mazingira, matumizi ya teknolojia na utekelezaji wa sheria ili kuhakikisha mazingira yanalindwa kwa manufaa ya kizazi cha sasa na vijavyo.









Hakuna maoni:

Chapisha Maoni

𝗡𝗘𝗠𝗖 𝗬𝗔𝗞𝗨𝗧𝗔𝗡𝗔 𝗡𝗔 𝗪𝗔𝗔𝗡𝗗𝗔𝗔𝗝𝗜 𝗪𝗔 𝗧𝗔𝗡𝗭𝗔𝗡𝗜𝗔 𝗚𝗥𝗘𝗘𝗡 𝗦𝗨𝗠𝗠𝗜𝗧 𝟮𝟬𝟮𝟲

Baraza la Taifa la Hifadhi na Usimamizi wa Mazingira (NEMC) limekutana na ujumbe wa waandaaji wa Tanzania Green Summit (TGS), inayotarajiwa ...