Nyumbani

KAMATI YA KUDUMU YA BUNGE YA MAJI NA MAZINGIRA YAKAGUA HALI YA MAZINGIRA DAMPO LA PUGU NA MTO NG’OMBE DAR ES SALAAM

Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Maji na Mazingira leo, Oktoba 17, 2026, imefanya ziara ya kukagua hali ya mazingira katika Dampo la Pugu Kinyamwezi na Mto Ng’ombe, Dar es Salaam, kwa lengo la kutathmini utekelezaji wa maagizo yaliyotolewa na Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Deogratius Ndejembi, Septemba 18, 2026, kuhusu hatua za kukabiliana na changamoto za kimazingira katika maeneo hayo.


Akizungumza baada ya ziara hiyo, Makamu Mwenyekiti wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Maji na Mazingira Mhe. Prof. Pius Zebhe Yanda (Mb) ameelekeza kuwepo kwa mpango madhubuti wa kudhibiti na kusimamia Dampo la Pugu na kusisitiza umuhimu wa kutathmini afya za wananchi wanaoishi karibu na eneo hilo ikiwa ni  pamoja na kuweka uzio ili kuhakikisha makazi ya Wananchi hayasogei karibu na dampo hilo 

Kwa upande wake Naibu Waziri Ofisi ya Makamu wa Rais (Mazingira) Mhe. Reuben Kwagilwa ameeleza kuwa Serikali haina budi kuweka mwekezaji atakayeshughulikia uchakataji wa taka katika Dampo la Pugu, hatua inayotarajiwa kuboresha usimamizi wa taka na kupunguza athari za kimazingira kwa wananchi wanaozunguka eneo hilo.

Aidha, ameielekeza Halmashauri ya Jiji la Dar es Salaam kushirikiana kwa karibu na taasisi zote zinazohusika, ikiwemo Baraza la Taifa la Hifadhi na Usimamizi wa Mazingira (NEMC), ili kuhakikisha mradi wa dampo hilo haukwami.

Awali Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam mhe. Albert Chalamila, akiwasilisha taarifa fupi kuhusu hali ya Mazingira amesema Mkoa wa Dar es Salaam una takribani kilomita za mraba 1300 na watu zaidi ya Milioni  tano na laki tatu kwa mujibu wa sensa ya Mwaka 2022 hali inayopelekea uzalishaji mkubwa wa taka kwa siku na kutokana miundombinu kupelekea kiwango kidogo cha taka kupelekea dampo.



Hakuna maoni:

Chapisha Maoni

KAMATI YA KUDUMU YA BUNGE YA MAJI NA MAZINGIRA YAKAGUA HALI YA MAZINGIRA DAMPO LA PUGU NA MTO NG’OMBE DAR ES SALAAM

Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Maji na Mazingira leo, Oktoba 17, 2026, imefanya ziara ya kukagua hali ya mazingira katika Dampo la Pugu Kinyam...