Baraza la Taifa la Hifadhi na Usimamizi wa Mazingira (NEMC) kwa kushirikiana na Taasisi za umma na binafsi waadhimisha siku ya mikoko duniani kwa kupanda miche takribani 1,000 ya miti ya Mikoko eneo la Kilongawima lililopo pembezoni mwa fukwe ya 'Mbezi beach' Halmashauri ya Kinondoni Manispaa ya Jijini Dar es.
Akizungumza mara baada ya zoezi la upandaji wa miche hiyo Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni Mhe. Saad Mtambule amewataka wananchi kulinda na kithamini mikoko kwani Inamanufaa mkubwa katika kulinda ikolojoa ya bahari na viumbe hai waishio majini.
Meneja wa Tafiti za Mazingira (NEMC) Dkt. Rose Sallema akiwa ameshika mche wa Mkoko tayari kwa kuupanda katika zoezi la upandaji Mikoko eneo la KilongawimaNaye Dkt.Rose Sallema, Meneja wa Tafiti za Mazingira (NEMC) alipozungumza alisema mikoko ni rasilimali ya bahari inayotakiwa kutunzwa kwani inafaida kiuchumi,kijamii na kimazingira.
Viongozi na wadau wa Mazingira wakitazama hati miliki ya TFS kuashiria ulinzi wa eneo la Kilongawima lililopandwa takribani miti ya Mikoko 1,000 Naye Mkurugenzi Msaidizi, Maendeleo ya Misitu kutoka Wizara ya Maliasili na Utalii ndugu. Seleboni Mushi alipozungumza aliitaka jamii kuzingatia Uhifadhi wa misitu ya Mikoko kwani husaidia kuhifadhi fukwe na hewa ukaa hivyo kusaidia kuhimili mabadiliko ya tabianchi.
Afisa Mazingira Mkuu Bi. Ritha Said akipanda mche wa Mkoko wakati wa zoezi la upandaji Mikoko eneo la Kilongawima Ameongeza kuwa ni Hifadhi ya viumbe hai na husaidia jamii hasa za Pwani katika kujipatia kipato.
Taasisi zilizoshiriki Maadhimisho hayo ni pamoja na TFS, WWF, IUCN, Wetland, Mwambao International Wawakilishi kutoka maeneo ya Pwani ya Kibiti, Kilwa na Mafia.
Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni ndugu. Saad Mtambule akizungumza na washiriki wote waliopanda miche ya Mikoko katika eneo la Kilongawimakatika kuadhimisha Siku ya Mikoko duniani
Zoezi la upandaji miti katika eneo la kilongawima likifanyika ikiwa ni sehemu ya Maadhimisho ya Siku ya Mikoko Duniani inayoadhimishwa tarehe 26 Julai kila mwaka ambapo kwa Tanzania imeadhimishwa tarehe 4 kwa kupanda Mikoko.