Baraza la Taifa la Hifadhi na Usimamizi wa Mazingira (NEMC) limeshiriki katika mafunzo ya matumizi ya teknolojia ya Remote Sensing na Geographic Information Systems (GIS) yanayolenga kuimarisha uwezo wa taasisi za Serikali katika usimamizi, ufuatiliaji na uhifadhi wa rasilimali za bahari na uvuvi yanayofanyika kwa muda wa siku nne kuanzia Februari 3 hadi 6, 2026, jijini Dar es Salaam.

Mafunzo hayo yameratibiwa na Korean Institute of Ocean Science and Technology (KIOST) kwa kushirikiana na Taasisi ya Utafiti wa Uvuvi Tanzania (TAFIRI) huku wadau zaidi ya 20 kutoka sekta ya Bahari na Uvuvi wanaotoka katika taasisi mbalimbali za Serikali zimeshiriki mafunzo hayo ikiwa ni pamoja na Baraza la Taifa la Hifadhi na Usimamizi wa Mazingira (NEMC), Taasisi ya Utafiti wa Uvuvi Tanzania (TAFIRI), Taasisi ya Utafiti wa Uvuvi Zanzibar (ZAFIRI), Dar es Salaam Maritime Institute (DMI), Chuo Kikuu cha Dar es Salaam (UDSM), Fisheries Education and Training Agency (FETA), Mamlaka ya Hali ya Hewa Tanzania (TMA), Deep Sea Fishing Authority (DSFA), pamoja na Wizara ya Mifugo na Uvuvi (MLF).
Aidha, Mafunzo haya ni sehemu ya jitihada za kuimarisha matumizi ya teknolojia ya satelaiti katika ukusanyaji na uchambuzi wa taarifa zitakazosaidia katika usimamizi endelevu wa rasilimali za bahari na uvuvi, pamoja na kukabiliana na athari za mabadiliko ya tabianchi.