Nyumbani

NEMC KUAINISHA FURSA ZILIZOPO KATIKA TAKA, MACHI 30

Ni katika Viwanja vya Mnazi mmoja Jijini Dar es Salaam, Maadhimisho ya Siku ya Kimataifa ya kuondoa Taka 

Baraza la Taifa la Hifadhi na Usimamizi wa Mazingira (NEMC) limejipanga kutoa elimu kuhusu fursa zilizopo kwenye taka katika Maadhimisho ya siku ya Kimataifa ya Kuondoa Taka yanayotarajiwa kuadhimishwa Machi 30, 2026 katika viwanja vya Mnazi mmoja Jijini Dar es Salaam.

Maadhimisho hayo yatatanguliwa na maonesho yatakayoanza tarehe 28 hadi siku ya kilele, Machi 30, 2026 yatakayobainisha namna ambavyo taka ni fursa kupitia ubunifu wa bidhaa zitokanazo na taka

Akizungumza na vyombo vya Habari, Meneja Uzingatiaji wa Sheria (NEMC) Bw. Hamadi Taimuru amesema siku hii inalenga kuhamasisha umma  kupunguza uzalishaji wa taka na kutoa elimu kwa wadau na wananchi wote kutambua fursa za uwekezaji katika taka kupitia ukusanyaji, uchakataji na Urejelezaji wa taka.

"Tunawaomba wananchi na wadau wote tufike katika viwanja vya Mnazi mmoja kuanzia saa mbili asubuhi hadi saa kumi na moja jioni kujifunza na kujionea fursa za uwekezaji katika eneo la taka". Amesema Bw. Taimuru

Aidha ameongeza kuwa Maadhimisho hayo yamelenga kuhimiza na kuhakikisha kuwa dhana ya 𝗣𝘂𝗻𝗴𝘂𝘇𝗮, 𝗧𝘂𝗺𝗶𝗮 𝘁𝗲𝗻𝗮 𝗻𝗮 𝗥𝗲𝗷𝗲𝗹𝗲𝘇𝗮 inatekelezwa kwa vitendo na kwa matakwa ya Sheria ili kuwa na Mazingira safi, afya bora ya jamii na matumizi ya rasilimali endelevu Kwa ajili ya Maendeleo ya Taifa.

Kauli mbiu ya kimataifa ya Maadhimisho haya ni "𝒌𝒖𝒘𝒆𝒛𝒆𝒔𝒉𝒂 𝒕𝒂𝒌𝒂 𝒔𝒊𝒇𝒖𝒓𝒊 𝒌𝒘𝒆𝒏𝒚𝒆 𝑺𝒆𝒌𝒕𝒂 𝒚𝒂 𝒄𝒉𝒂𝒌𝒖𝒍𝒂" ambayo inaangazia tatizo la upotevu wa chakula Duniani na Athari zake kwa Mazingira na Jamii ambapo inakadiriwa kuwa upotevu wa chakula huchangia takribani asilimia kumi (10%) ya hewa chafuzi (greenhouse gases)

Ameongeza kuwa, kitaifa inaendelea Kaulimbiu ya '𝑻𝒂𝒌𝒂 𝒏𝒊 𝑭𝒖𝒓𝒔𝒂' ambayo inaweka msisitizo kuwa taka si taka tu bali ni malighafi za kutengeneza bidhaa nyingine.

DKT. FESTO DUGANGE AITIKISA KAGERA, AITAKA NEMC KUKAZA UZI USIMAMIZI WA SHERIA ZA MAZINGIRA KWENYE MIRADI

Naibu Waziri Ofisi ya Makamu wa Rais (Muungano na Mazingira), Mhe.Dkt. Festo Dugange, amelitaka Baraza la Taifa la Hifadhi na Usimamizi wa Mazingira (NEMC) kuhakikisha linasimamia kikamilifu utekelezaji wa Sheria ya Usimamizi wa Mazingira katika miradi yote ya maendeleo inayotekelezwa mkoani Kagera, ili kulinda rasilimali za mazingira na afya za wananchi.

Akizungumza wakati wa ziara ya kukagua miradi ya mazingira katika Halmashauri za Wilaya ya Karagwe na Misenyi, Dkt. Dugange alisisitiza kuwa NEMC inapaswa kuimarisha ukaguzi na ufuatiliaji wa miradi, kuhakikisha tathmini za athari kwa mazingira (EIA) zinafanyika kwa mujibu wa sheria na kwamba masharti yote ya kimazingira yanazingatiwa kabla na wakati wa utekelezaji.

Katika ziara hiyo, Naibu Waziri alikagua mradi wa vijana wa kuchakata taka za plastiki unaosaidia kupunguza uchafuzi wa mazingira na kutoa ajira kwa vijana. Pia alitembelea mradi wa biashara ya kaboni kupitia kilimo mseto (Kinoni Agroforestry Farm) unaotekelezwa na kampuni ya KADERES, unaolenga kuwawezesha wakulima kunufaika na biashara ya hewa ukaa sambamba na kuhifadhi mazingira.

Aidha, alikagua Kiwanda cha Vifungashio (Magunia) cha KADERES, Mradi wa Nishati Safi ya Kupikia unaohamasisha matumizi ya nishati mbadala ili kupunguza ukataji miti, pamoja na mradi wa ujenzi wa dampo la kuhifadhia maji taka wilayani Karagwe unaolenga kuboresha usafi wa mazingira na kulinda afya ya jamii.

Akizungumza na wananchi wa Karagwe na Misenyi, Dkt. Dugange alihamasisha jamii kuona mazingira kama fursa ya kiuchumi. Alieleza kuwa taka zinaweza kuwa rasilimali yenye thamani endapo zitasimamiwa na kuchakatwa kwa usahihi.

“Taka si taka tu bali ni rasilimali muhimu inayoweza kuleta manufaa ya kiuchumi. Taka zinazooza zinaweza kutumika kutengeneza gesi na mbolea ya asili kwa ajili ya bustani za kioganiki na kulinda rutuba ya udongo,” amesema.

Kwa upande wake, Meneja NEMC Kanda ya Ziwa Victoria Magharibi Bw. Boniphace Guni, amesema NEMC itaendelea kuimarisha usimamizi wa miradi yote inayotekelezwa katika kanda hiyo na kuhakikisha sheria za mazingira zinatekelezwa kikamilifu nchini kote.

Ziara hiyo pia ilihusisha ushiriki wa Halmashauri ya Wilaya ya Karagwe na Halmashauri ya Wilaya ya Misenyi, ikiwa ni sehemu ya juhudi za Serikali za kuhakikisha maendeleo endelevu yanakwenda sambamba na uhifadhi wa mazingira.

NEMC KANDA YA MOROGORO/RUFIJI NA MORUWASA WAPANDA MITI 5,000

NEMC Kanda ya Morogoro/Rufiji imeshirika zoezi la kupanda miti 5,000 aina ya Mkongo ( Afzelia quanzensis) katika eneo la bwawa la Mindu, Kata ya Kauzeni Manispaa ya Morogoro. Zoezi lililoandaliwa na Mamlaka ya Maji Safi na Usafi wa Mazingira Morogoro (MORUWASA) kama sehemu ya maadhimisho ya wiki ya Maji.



NEMC YASHIRIKI ZIARA YA KATIBU MKUU DKT. RICHARD MUYUNGI-KAGERA

Baraza la Taifa la Hifadhi na Usimamizi wa Mazingira (NEMC) – Kanda ya Ziwa Victoria Magharibi, limeshiriki ziara ya Katibu Mkuu, Ofisi ya Makamu wa Rais (Muungano na Mazingira), Dkt. Richard Muyungi, iliyofanyika mkoani Kagera tarehe 16.03.2026, kwa lengo la kufuatilia utekelezaji wa maagizo ya Serikali kuhusu matumizi ya nishati safi na uhifadhi wa mazingira.

Katika ziara hiyo, Dkt. Muyungi alitembelea Shule ya Sekondari Rugambwa iliyopo Manispaa ya Bukoba pamoja na Shule ya Msingi Hosiana iliyopo Wilaya ya Karagwe. Lengo la ziara hizo lilikuwa kujionea namna taasisi za elimu zinavyotekeleza maagizo ya Mheshimiwa Rais, Dkt. Samia Suluhu Hassan, kuhusu kuhamia matumizi ya nishati safi ili kupunguza uzalishaji wa hewa ukaa unaochangia mabadiliko ya tabianchi.

Aidha, Katibu Mkuu alitembelea mradi wa Kaderes Enterprise uliopo Wilaya ya Kyerwa, mkoani Kagera, ambapo alipata fursa ya kujionea juhudi za wadau katika utekelezaji wa miradi ya kaboni (carbon credit) inayolenga kupunguza uzalishaji wa gesi chafuzi na kuchangia katika uhifadhi wa mazingira.

Katika ziara hiyo, Dkt. Muyungi alisisitiza masuala mbalimbali kama vipaumbele vya kitaifa:

- Matumizi ya Nishati Safi: Kuimarisha matumizi ya nishati mbadala kama vile majiko banifu, gesi asilia, nishati ya jua na umeme safi ili kupunguza utegemezi wa kuni na mkaa, kulinda misitu, na kuboresha afya ya jamii.

- Udhibiti wa Hewa Ukaa: Kupunguza uzalishaji wa gesi chafuzi (GHGs) kupitia teknolojia rafiki kwa mazingira, ufanisi wa matumizi ya nishati, na utekelezaji wa miradi ya upandaji miti na uhifadhi wa misitu.

- Biashara ya Kaboni: Kukuza uelewa na ushiriki wa wadau katika miradi ya Kaboni kama fursa ya kiuchumi, ambapo jamii na taasisi zinaweza kunufaika kifedha kupitia uhifadhi wa mazingira na kupunguza uzalishaji wa hewa ukaa.

- Ushirikishwaji wa Taasisi zenye zaidi ya watu 100: Kuhamasisha taasisi za serikali na zisizokuwa za serikali zenye watu zaidi ya 100 kuwa vinara wa matumizi ya nishati safi na elimu ya mazingira kwa vitendo.

-Pamoja na  Uzingatiaji wa Sera na Sheria: Kusisitiza uzingatiaji wa miongozo na Sheria za Mazingira.

NEMC NA WATER AIDS WAADHIMISHA SIKU YA MAJI

Baraza la Taifa la Hifadhi na Usimamizi wa Mazingira (NEMC), kwa kushirikiana na shirika lisilo la kiserikali la WaterAid, katika kuadhimisha mwezi wa maji mwezi Machi na Siku ya urejelezaji Duniani (Global Recycling Day, tarehe 18 Machi), kuelekea kilele cha Siku ya Kimataifa ya Taka Sifuri (International Day of Zero Waste), limefanya tathmini ya hali ya udhibiti wa taka ngumu kwa lengo la kulinda chanzo cha maji cha Ziwa Bassotu kilichopo Kijiji cha Bassotu, Wilaya ya Hanang, Mkoa wa Manyara.

Tathmini hiyo imelenga kubaini changamoto zilizopo na kuweka mikakati bora ya udhibiti wa taka ndani ya kijiji hicho na maeneo jirani, ili kunusuru ziwa hilo ambalo kwa sasa linakabiliwa na hatari ya kugeuzwa dampo lisilo rasmi. Hali hii inachangiwa na utupaji holela wa taka ngumu, ikiwemo chupa za viuatilifu vinavyotokana na shughuli za kilimo, jambo linalohatarisha ubora wa maji, uhai wa viumbe hai ziwani na afya ya binaadamu na mazingira kwa ujumla.

Malengo hayo yanaweza kufikiwa endapo tutaimarisha utekelezaji wa dhana ya uchumi mzunguko (circular economy) kuelekea taka sifuri kupitia urejelezaji. Hatua hii itasaidia kulinda chanzo hicho cha maji na kuboresha hali ya mazingira ya Kijiji cha Bassotu kwa ujumla.

MATUKIO KATIKA PICHA, UKAGUZI WA MGODI WA DHAHABU WA GEITA GOLD MINES (GGM) KATIKA ZIARA YA MHESHIMIWA WAZIRI, MHANDISI HAMAD YUSUF MASAUNI MKOANI GEITA

Pichani ni ziara ya Mheshimiwa Waziri wa nchi Ofisi ya Makamu wa Rais (Muungano na Mazingira) Mhandisi Hamad Yusuf Masauni (wa kwanza kushoto) akikagua hali ya Mazingira katika Mgodi wa Dhahabu wa Geita Gold Mines Mkoani Geita ambapo aliambatana na Mkurugenzi Mkuu wa NEMC Dkt. Immaculate Sware Semesi na baadhi ya watumishi wa NEMC, pamoja na Viongozi wengine kutoka Ofisi ya Makamu wa Rais Machi 14, 2026










MATUKIO KATIKA PICHA, WAZIRI MASAUNI (OFISI YA MAKAMU WA RAIS-MUUNGANO NA MAZINGIRA APANDA MTI KATIKA KITUO CHA ELIMU YA ZEBAKI CHA NEMC-GEITA

Waziri wa nchi ofisi ya makamu wa Rais (Muungano na Mazingira) Mhandisi Hamad Masauni akipanda mti katika eneo litakapokuwa lango kuu la Jengo la Kituo cha kutoa elimu kuhusu Athari za matumizi ya Zebaki (Mercury) katika uchenjuaji Madini ya Dhahabu katika afya na Mazingira linalosimamiwa na NEMC chini ya ufadhili wa Global Environmental Facility (GEF) lililojengwa mkabala na Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Geita ikiwa ni jitaha za kuunga mkono  azma ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania za kukijanisha Tanzanaia.

Mhe. Waziri amepanda mti huo wakati wa ziara yake alipotembelea Jengo hilo.

Kadhalika katika kuunga mkono jitihada hizo Katibu Mkuu, Ofisi ya Makamu wa Rais (Muungano na Mazingira) Dkt. Richard Muyungi pia alipanda mti katika eneo hilo







𝗡𝗘𝗠𝗖 𝗬𝗔𝗢𝗡𝗚𝗢𝗭𝗔 𝗠𝗔𝗝𝗔𝗗𝗜𝗟𝗜𝗔𝗡𝗢- 𝗪𝗔𝗥𝗦𝗛𝗔 𝗬𝗔 𝗞𝗜𝗞𝗔𝗡𝗗𝗔 𝗞𝗔𝗧𝗜 𝗬𝗔𝗞𝗘 𝗡𝗔 𝗖𝗦𝗘 𝗡𝗔 𝗜𝗡𝗗𝗜𝗔

 𝗡𝗶 𝗞𝗮𝘁𝗶𝗸𝗮 𝗙𝘂𝗿𝘀𝗮 𝘇𝗶𝗹𝗶𝘇𝗼𝗽𝗼 𝗸𝘄𝗲𝗻𝘆𝗲 𝗨𝘀𝗶𝗺𝗮𝗺𝗶𝘇𝗶 𝘄𝗮 𝘁𝗮𝗸𝗮 𝘇𝗮 𝗠𝗮𝘁𝗮𝗶𝗿𝗶 𝗖𝗵𝗮𝗸𝗮𝘃𝘂 Baraza la Ta...