Nyumbani

NEMC YAFANYA UFUATILIAJI WA MRADI WA KCCMP

Baraza la Taifa la Usimamizi wa Mazingira (NEMC) limefanya ufuatiliaji wa baada ya utekelezaji wa Mradi wa Uhifadhi na Usimamizi wa Bonde la Kihansi (KCCMP) kuanzia tarehe 19 hadi 30 Januari 2026 katika wilaya za Mlimba, Kilolo na Mufindi.

Mradi huo ulitekelezwa kati ya 2013 hadi 2019, ukiwa na lengo la kuimarisha uhifadhi wa bioanuai na kulinda viumbe hai adimu kama Chura wa Kihansi (Kihansi Spray Toad), sambamba na kusimamia rasilimali za maji kwa uendelevu.

Timu ya NEMC iliongozwa na Bw. Paul Kalokola, ikishirikiana na maafisa wa halmashauri na taasisi kama UDSM, SUA, TAWIRI, TANESCO na Ofisi ya Bonde la Rufiji. Walitembelea vituo vya uzalishaji na urejeshwaji wa Chura wa Kihansi na maeneo ya mradi kujionea utekelezaji.

Ripoti ya NEMC itatoa mapendekezo ya kitaalamu kuhakikisha uendelevu wa matokeo ya mradi na uhifadhi wa Bonde la Kihansi kwa muda mrefu.













WAALAMU WA KUDHIBITI MATUMIZI YA ZEBAKI KWA WACHIMBAJI WADOGO (NEMC) NA WATAALAMU KUTOKA BENKI YA DUNIA WAKUTANA NA DKT. MUYUNGI

 

Timu ya wataalamu kutoka Baraza la Taifa la Hifadhi na Usimamizi wa Mazingira (NEMC) inayosimamia Mradi wa Kudhibiti Matumizi ya Zebaki kwa Wachimbaji Wadogo wa Dhahabu (EHPMP) wakiongozwa na Mratibu wa mradi huo Mhandishi Dkt. Befrina Igulu wakiwa na timu ya wataalamu kutoka Benki ya Dunia wamekutana na Katibu Mkuu Ofisi ya Makamu wa Rais (Muungano na Mazingira) Dkt. Richard Muyungi Februari 2,2026 kwenye Ofisi zilizopo katika jengo la NHIF jijini Dodoma.

Wataalamu hao NEMC na Benki ya Dunia wamekutana na Dkt. Muyungi kwa lengo la kutathmini uendelevu wa mradi na kuhakikisha uzingatiaji wa mikataba ya kimataifa.

Aidha, majadiliano yaligusia upatikanaji wa rasilimali fedha za ziada kwa ajili ya usimamizi wa taka za kielektroniki ambazo zina uhusiano wa karibu na athari za madini joto kama zebaki.

Benki ya Dunia na Katibu Mkuu Ofisi ya Makamu wa Rais (Muungano na Mazingira) Dkt. Richard Muyungi kwa pamoja wamepongeza hatua zilizofikiwa katika kutimiza malengo ya msingi ya utekelezaji wa mradi huu.

#ehpmp #environmentalhealth #worldbank #mercuryfree







NEMC, HALMASHAURI YA JIJI LA DAR ES SALAAM NA WADAU WA MAZINGIRA WASAFISHA FUKWE YA DENGU

Baraza la Taifa la Hifadhi na Usimamizi wa Mazingira (NEMC) Kanda ya Ilala  limeshirikiana na Halmashauri ya Jiji la Dar es Salaam pamoja na wadau mbalimbali wa Mazingira kusafisha fukwe ya Dengu iliyopo Kata ya Kivukoni, Wilaya ya Ilala, Jijini Dar es Salaam.

Zoezi hilo lililofanyika leo Januari 31, 2026 lililenga kuimarisha usafi wa mazingira na kulinda fukwe dhidi ya uchafuzi pamoja na kuboresha mandhari ya jiji, hususan Wilaya ya Ilala ambayo ni lango kuu la kupokea wageni wanaoingia nchini kupitia Kiwanja cha Ndege cha Kimataifa cha Julius Nyerere, Bandari ya Dar es Salaam pamoja na Stesheni ya Treni.

Mgeni rasmi katika zoezi hilo alikuwa Mkuu wa Wilaya ya Ilala, Mheshimiwa Edward Mpogolo, ambaye amesisitiza umuhimu wa kuendeleza usafi wa mazingira kwa ushirikiano wa karibu kati ya Serikali, taasisi na wadau mbalimbali ili kuhakikisha Wilaya ya Ilala inaendelea kuwa safi, salama na yenye kuvutia.

Amesema ushiriki wa wadau katika shughuli za usafi wa mazingira ni nguzo muhimu ya kulinda afya za wananchi, kuhifadhi mazingira ya fukwe na kuchangia maendeleo endelevu ya jiji na taifa kwa ujumla.




NEMC YAWAJENGEA UWEZO WATUMISHI WAKE KATIKA MAWASILIANO NA VYOMBO VYA HABARI

Baraza la Taifa la Hifadhi na Usimamizi wa Mazingira (NEMC) leo Februari 2, 2026 limewawezesha watumishi wake kwa kuwapatia mafunzo ya namna bora ya kuwasiliana na vyombo vya habari, yaliyofanyika katika ofisi za NEMC jijini Dar es Salaam.

Mafunzo hayo yalitolewa na mwezeshaji Dkt. David Mrisho (PhD) ambaye ni Mhadhiri Mwandamizi na Mkuu wa Idara ya Mahusiano ya Umma na Masoko katika Chuo Kikuu cha Mtakatifu Augustine (SAUT), yakilenga kuwaimarisha watumishi katika utoaji wa taarifa sahihi, zenye ujumbe mmoja na unaoeleweka kwa umma kupitia vyombo vya habari.

Katika mafunzo hayo, mwezeshaji alieleza mbinu ya “3 Key Message Rule”, inayosaidia katika uwasilishaji wa taarifa kwa kujikita kwenye maswali muhimu ya nini kilitokea, nini kinafanyika kwa sasa, na nini kitaendelea kufanyika.

Aidha, washiriki walifundishwa matumizi ya mbinu ya “bridging technique” wakati wa kujibu maswali ya waandishi wa habari, ili kuhakikisha majibu yanabaki kuakisi ujumbe mkuu wa taasisi bila kupotosha mwelekeo wa mawasiliano.

Mafunzo hayo ni sehemu ya jitihada za NEMC za kuimarisha uwazi, uwajibikaji na ufanisi wa mawasiliano ya taasisi, hususan katika masuala ya uhifadhi na usimamizi wa mazingira kwa maendeleo endelevu ya Taifa.




NEMC YATAMBUA USHIRIKIANO KATI YAKE NA JESHI LA POLISI

Yashiriki mahafali ya kumi ya programu za vyuo vya polisi

Baraza la Taifa la Hifadhi na Usimamizi wa Mazingira (NEMC) limetambua mchango wa jeshi la polisi ulionao katika Utekelezaji wa Sheria ya Mazingira hasa suala la ulinzi na usalama kwa maafisa wakati wa ukaguzi, kudhibiti ukaidi na kuhakikisha hatua za kisheria zinachukuliwa katika masuala ya Mazingira nchini.

Hayo yamedhihirika wakati wa mahafali ya kumi ya programu za vyuo vya polisi yaliyofanyika Januari 29, 2026 katika viwanja vya chuo cha taaluma ya polisi Jijini Dar es Salaam ambapo Mkurugenzi Mkuu wa NEMC Dkt.Immaculate Sware Semesi ameshiriki.

Ushiriki wake ni muhimu katika kutambua mchango ilionao wa kuimarisha utekelezaji wa Sheria za Mazingira nchini kwani uhalifu wa kimazingira kama kelele chafuzi, uharibifu wa mazingira na biashara haramu ya taka hudhibitiwa kwa ufanisi zaidi hali inayoongeza utii wa Sheria, kurahisisha uchunguzi na uwasilishaji wa kesi mahakamani.

DKT. SEMESI AKAGUA UTEKELEZAJI WA MRADI WA KUDHIBITI MATUMIZI YA ZEBAKI

Mkurugenzi Mkuu wa Baraza la Taifa la Hifadhi na Usimamizi wa Mazingira (NEMC), Dkt. Immaculate Sware Semesi, amefanya ziara ya kukagua utekelezaji wa Mradi wa Kudhibiti Matumizi ya Zebaki kwa Wachimbaji Wadogo wa Dhahabu (EHPMP) katika maeneo mbalimbali ya uchimbaji mdogo.

Katika ziara hiyo, alitembelea mwalo wa mfano wa matumizi salama ya dhahabu unaojengwa llindi, kata ya Mwime wilayani Kahama; kituo cha teknolojia mbadala ya zebaki kijijini Bumva, kata ya Segese, Halmashauri ya Msalala; pamoja na kituo cha elimu ya kudhibiti matumizi ya zebaki kinachojengwa katika Halmashauri ya Mji wa Geita.


Aidha, Dkt. Semesi alikutana na Katibu Tawala wa Mkoa wa Geita, Ndugu Mohamed J. Gombati, na kujadili changamoto za mazingira pamoja na umuhimu wa kuanzishwa kwa Ofisi mpya ya kikanda ya NEMC mkoani Geita inayohudumia mikoa ya Geita, Shinyanga na Kagera.

Dkt. Semesi pia alisisitiza ushirikiano wa dhati katika kuhakikisha shughuli za kiuchumi zinaendelezwa sambamba na ulinzi endelevu wa mazingira.










KAMATI YA KITAIFA INAYOSHAURI MASUALA YA UTAFITI WA MAZINGIRA (ERAC) YAKUTANA KUPITISHA RASIMU YA MWONGOZO WA TAFITI ZA KIMAZINGIRA NCHINI

Kamati ya Taifa ya Ushauri wa Tafiti za Mazingira (Environmental Research Adivisory Committee - ERAC) yakutana mkoani Morogoro kufanya mapitio na kupitisha Rasimu ya Mwongozo wa Tafiti za Mazingira (National Environmental  Research Agenda - NERA) kupitia kikao chake cha siku mbili tarehe 29 na 30, Januari 2026 katika ukumbi wa mikutano wa EDEMA.

Akizungumza Mkurugenzi wa Usimamizi na Tafiti za Mazingira (DERM) kutoka Baraza la Taifa la Hifadhi na Usimamizi wa Mazingira (NEMC), Dkt. Menan Jangu wakati wa ufunguzi kwa niaba ya Mkurugenzi Mkuu wa NEMC, amesema mazingira ni suala mtambuka hivyo Mwongozo huu wa Tafiti za Mazingira ni muhimu sana katika kupata taarifa sahihi ambazo zinasaidia katika kufanya maamuzi juu ya maendeleo endelevu nchini.

Dr. Menani alifafanua kuwa “Ustawi wa Maisha yetu ya kila siku,, Uchumi wetu na masuala mbalimbali ya kijamii yanategemea afya ya mazingira; hivyo utunzaji wa mazingira yanatoa uhakika wa afya ya jamii lakini pia maendeleo endelevu ya shughuli za kila siku.

Aidha, alifafanua kuwa ili kufikia malengo ya Dira ya Taifa ya 2050 ni lazima kuwa na miongozo sahihi wa Tafiti za Mazingira ambayo itapatikana kwa kushirikisha wadau mbalimbali.

“Dira inatekelezwa kwa kuwa na miongozo au nyenzo mbalimbali ikiwemo suala zima la utafiti wa mazingira kupitia Agenda ya mazingira."

Aidha, alifafanua kuwa kamati hii inaundwa na wataalam wabobevu kutoka katika Taasisi za Elimu ya Juu, Wizara, Idara za serikali, kutoka katika sekta binafsi na mashirika yasiyo ya serikali; hivyo ni matarajio Rasimu ya Agenda inayojadiliwa itakuwa na uzito wa kipekee na kuwa nyezo sahihi katika utekelezaji wa Dira 2050.

Akizungumza Meneja wa Tafiti za Mazingira ambaye pia ni Mratibu wa Agenda ya Taifa ya Tafiti za Mazingira, Dkt. Rose Mtui amesema Agenda hiyo inatarajiwa kutolewa mwaka huu 2026 na huwa inadumu kwa kipindi cha miaka mitano kabla ya kupitiwa upya kwa lengo la kuingiza mambo mapya yanayojitokeza au mabadiriko ya sera na sharia mbalimbali.

Alibainisha kuwa, Rasimu ya agenda hii imetengenezwa kwa kuzingatia mambo mengi ikiwemo masuala mapya kama vile Uchumi wa Blue, Mabadiliko ya tabia nchi, Tekinolojia mpya (AI), changamoto ya utupaji holela wa plastiki, Kelele na Mitetemo nk. Pia Rasimu ya agenda imezingatia mambo mbalimbali ya Kisera, Dira ya Taifa, ilani ya Uchaguzi nk. Aidha, alisema kuwa rasimu hii imepitia gazi mbalimbali ambapo wadau walipata fulsa ya kupitia agenda iliyopita (NERA 2017-2022) na kufanya tathmini ya utekelezaji wa Agenda hiyo na kuibua mambo mapya ambayo yanatakiwa kuwekewa vipaumbele.




NEMC YASHIRIKI KIKAMILIFU KONGAMANO LA ANWANI ZA MAKAZI NA MAONESHO YA TEKNOLOJIA ZA POSTA 2026

Baraza la Taifa la Hifadhi na Usimamizi wa Mazingira (NEMC) limeshiriki kikamilifu Kongamano la Mwaka la Anwani za Makazi na Maonesho ya Hud...