Nyumbani

NEMC NA MWAKILISHI KUTOKA ULAYA WAJADILI NA MJUMBE KUTOKA ULAYA USIMAMIZI WA MAZINGIRA KATIKA SEKTA YA MADINI


Mkurugenzi wa Tathmini ya Athari kwa Mazingira na Jamii Bi. Lilian Lukambuzi (wa pili kushoto) akiwa katika picha ya pamoja na muwakilishi wa ujumbe wa Umoja wa Ulaya nchini Tanzania Meneja wa Programu (Utawala wa kiuchumi) Bw. Sebastian Schaber. Wa kwanza kushoto ni Kaimu Meneja wa Mapitio ya Tathmini ya Athari kwa Mazingira na Jamii (NEMC) Mha. Luhuvilo Mwamila. Wa kwanza kulia ni Meneja Usajili wa Wataalam elekezi wa Mazingira (NEMC) Bi. Edika Masisi. 

Baraza la Taifa la Hifadhi na Usimamizi wa Mazingira (NEMC) limekutana na muwakilishi wa ujumbe wa Umoja wa nchi za Ulaya (EU) nchini Tanzania na kujadili namna Tathmini ya Athari kwa Mazingira na Jamii zinavyofanyika kwa Tanzania na jinsi wanavyoweza kushirikiana na Baraza hususani katika masuala ya kimazingira kwa upande wa Sekta ya madini hasa madini muhimu (Critical Minerals) 

Kikao hiki kilijadili miongozo iliyopo  na kuainisha maeneo yanayohitaji usaidizi wao ili kuwezesha uzingatiaji wa Sheria kwa miradi ya madini inayowekezwa nchini.


Hakuna maoni:

Chapisha Maoni

MKUTANO WA 48 WA KAMATI YA URITHI WA DUNIA WA UNESCO WAHITIMISHWA RASMI BUSAN, JAMHURI YA KOREA

Tarehe 29 Julai 2026, ulihitimishwa rasmi Mkutano wa 48 wa Kamati ya Urithi wa Dunia wa UNESCO (48th Session of the World Heritage Committee...