Baraza la Taifa la Hifadhi na Usimamizi wa Mazingira (NEMC) limeshiriki kikamilifu Kongamano la Mwaka la Anwani za Makazi na Maonesho ya Huduma za Posta kwa kutoa elimu ya Mazingira kwa wadau walioshiriki katika Kongamano hilo.
Kongamano hilo limehitishwa rasmi leo Februari 8, 2026 na Mgeni Rasmi Waziri wa Mawasiliano na Teknolojia ya Habari Mhe. Angellah Jasmine Mbelwa Kairuki (Mb) ambapo ameeleza umuhimu wa matumizi ya mfumo wa Anwani za Makazi (NAPA) na kusisitiza matumizi ya mfumo huo ili kuwezesha utambuzi wa makazi na Maeneo ambayo shughuli za kiuchumi zinazohitaji ufuatililiaji zinafanyika.
Kongamano hilo lililobeba kauli mbiu isemayo "𝘼𝙣𝙬𝙖𝙣𝙞 𝙈𝙖𝙝𝙞𝙧𝙞 𝙣𝙖 𝙐𝙗𝙪𝙣𝙞𝙛𝙪 𝙬𝙖 𝙃𝙪𝙙𝙪𝙢𝙖 𝙯𝙖 𝙋𝙤𝙨𝙩𝙖 𝙠𝙬𝙖 𝙐𝙠𝙪𝙖𝙟𝙞 𝙅𝙪𝙢𝙪𝙞𝙨𝙝𝙞" lilianza Februari 5 na kuhitimishwa rasmi leo Februari 8, 2026 ambapo Kongamano hilo limefanyika kuanzia Februari katika Ukumbi wa wa Kimataifa wa Julius Nyerere (JNICC) Jijini Dar es salaam.