Wito juu ya mambo makubwa mawili watolewa na Kaimu Mkurugenzi wa Tafiti za Mazingira wa Baraza la Taifa la Hifadhi na Usimamizi wa Mazingira (NEMC) Dkt. Careen Kahangwa kwa niaba ya Mkurugenzi Mkuu wa NEMC Dkt. Immaculate Sware Semesi aliyekuwa Mgeni Rasmi katika hafla ya kufunga Mkutano wa Tanzania Green Summit 2026 ukiofanyika katika Ukumbi wa Mlimani City jijini Dar es Salaam.
Dkt. Careen amesema jambo la kwanza ni kujenga mfumo wa kugeuza ubunifu na fursa za mazingira kuwa miradi inayotekelezeka, inayoweza kufadhiliwa na inayoweza kukua. Akisisitiza kuwa hii inamaanisha kuunganisha wabunifu, wajasiriamali na jamii na ujuzi, teknolojia, masoko, taasisi za fedha na washirika wa maendeleo.
Amesema, "hatupaswi kuridhika kuona mawazo mazuri yakibaki kwenye mashindano, maonesho au miradi ya majaribio. Tunahitaji kuyaona yakibadilika kuwa biashara endelevu, ajira, uwekezaji na suluhisho kwa changamoto za mazingira na tabianchi."
Amesema jambo la pili ni kujenga ushirikiano wa kudumu
unaotafsiri maazimio ya kongamano hili kuwa hatua na matokeo yanayopimika.
Akisisitiza kuwa Tanzania Green Summit isiwe tukio la siku mbili pekee, bali
iwe sehemu ya mchakato unaoendelea wa kuunganisha sera, ubunifu, fedha,
teknolojia na utekelezaji.
Ameongeza, "Tunahitaji kufuatilia fursa zilizojadiliwa, kuendeleza ushirikiano ulioanzishwa na kupima matokeo ya hatua zitakazochukuliwa baada ya kongamano hili."
Tanzania Green Summit 2026 imefanyika kwa siku mbili kuanzia trh 15 hadi 16 Septemba, 2026 ikiwa na kaulimbiu isemayo "Turning Climate Action into Opportunity" ikiwa na maana ya Kugeuza Hatua za Kukabiliana na Mabadiliko ya Tabianchi kuwa Fursa.



.jpeg)




.jpeg)

Hakuna maoni:
Chapisha Maoni