Baraza la Taifa la Usimamizi wa Mazingira (NEMC) lilishiriki katika Kongamano la Biashara na Uwekezaji kati ya Umoja wa Ulaya na Tanzania lililofanyika kuanzia tarehe 28 Septemba hadi 6 Oktoba 2026 nchini Finland, Italia, Uholanzi na Ubelgiji. Kongamano hilo liliwakutanisha wawakilishi wa Serikali, taasisi za umma, sekta binafsi na wafanyabiashara kujadili fursa za biashara na uwekezaji katika sekta mbalimbali, zikiwemo madini, kilimo, TEHAMA na bandari.
Miongoni mwa masuala yaliyojadiliwa ni uchumi mzunguko
(Circular Economy), Mazingira, Jamii na Utawala Bora (ESG), pamoja na usimamizi
wa taka zinazotokana na shughuli za uchimbaji na uchakataji wa madini muhimu
(Critical Minerals), vifaa vya umeme na kielektroniki. NEMC ilishiriki katika
mijadala ya jopo nchini Finland na Uholanzi kuhusu fursa za uwekezaji katika
sekta ya madini muhimu na vipaumbele vya kimkakati vya Tanzania.
Katika mijadala hiyo, NEMC ilieleza umuhimu wa kuzingatia masuala ya ESG, matakwa ya kimazingira na ufuatiliaji wa mnyororo wa thamani wa madini. Ilisisitizwa kuwa uzingatiaji wa viwango hivyo unaweza kuimarisha ushindani wa Tanzania katika masoko ya kimataifa na kuongeza uaminifu wa wawekezaji.
Aidha, NEMC ilieleza kuwa usimamizi madhubuti wa mazingira na utekelezaji wa kanuni za ESG ni muhimu katika kuvutia uwekezaji endelevu, kuongeza thamani ya madini yanayozalishwa nchini na kupunguza athari za kimazingira zinazotokana na shughuli za uchimbaji na uchakataji.
Kwa ujumla, ushiriki wa NEMC katika kongamano hilo uliwezesha kubadilishana uzoefu na wadau wa kimataifa na kuwasilisha nafasi ya usimamizi wa mazingira katika kukuza uwekezaji endelevu. Pia, ulitoa fursa ya kuonesha namna uzingatiaji wa masuala ya mazingira, ESG na uchumi mzunguko unavyoweza kuchangia katika kuongeza thamani ya rasilimali za Tanzania na kuimarisha ushindani wake katika masoko ya kimataifa.




.jpeg)

.jpeg)
.jpeg)
.jpeg)
.jpeg)

.jpeg)

.jpeg)
.jpeg)
.jpeg)
.jpeg)

.jpeg)



.jpeg)
.jpeg)
.jpeg)

.jpeg)















.jpeg)

